Wednesday, August 28, 2019

#USOPEN_VIGOGO CHALI

SIKU Safi  kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson  na kutinga raundi ya Pili.
 - Rafael Nadal  akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululizo bila majibu .
- Mcanada Dennis Shapovalov yeye alikua na siku nzuri mbele ya Bwanamdogo Auger aliasime kwa "Straight set "
- Ni kama Wilfred Tsonga bado hajarudi vizuri toka atoke kwenye Majeraha , akiaga raundi ya awali mbele ya Sandgren .
- Moja ya watu waliopewa nafasi kubwa kuleta ushindani dhidi ya Miamba mitatu " Big 3" ( Novak , Nadal na Federer)
Dominic Thiem amepoteza mchezo dhidi ya Thamos Fabbiano baada mechi ndefu ikichukua seti 4.

 Tuendelee kuwa Pamoja ...


US OPEN YAPAMBA MOTO

LABDA Media  zinamjengea Presha Binti  Coco Gauff , akiwa na umri wa miaka 15 tayari anapewa " Hype" .
 haikua shida kwa Mrusi Anastasia Potapova kutinga raundi ya pili mbele ya Mmarekani Coco Gauff.
- Venus Williams atamvaa mukraine Elina Svitolina , wakati  Mwanadada Catheline McNailly  atavaa kigingi dhidi ya Serena Williams  kunako raundi ya Pili.
- Bingwa wa michuano ya Wimbledon Simona Halep   hapo jana aliibuka na ushindi wa kwanza wa US Open  toka mwaka 2016 . Kwamba tangu mwaka 2016 hakuwai vuka raundi ya kwanza .

-  Bianca Vannesa  yeye alikua na siku  safi mbele ya binti Volynets  baada ya ushindi wa " Straight set " 6-2, 6-4.
- Naomi Osaka ameanza kwa tabu dhidi Anna Blinkova , akisonga mbele katika seti ya Mwisho (6-4,6-7(5),6-2 .

Taifa la Belarus walishuhudia Aryna Sabarenka akimchapa Vick Azarenka na Aryna kusonga mbele kunako US Open .


Friday, August 23, 2019

TAIFA STARS HAZARANI

Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo wa kuwania kuingia kwenye makundi ya kugombania kufuzu kombe la dunia


Huku akiwajumuisha wachezaji Ally N'yanzi anae cheza timu ya Minnesota inayo shiliki ligi marekani na Eliuter Mpepo anae cheza ligi ya Zambia timu Buildcon

Thursday, August 22, 2019

#BREAKING_NEWS JUNIOR AGOGO AFARIKI

#BREAKING_NEWS Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana Junior Agogo amefariki dunia akiwa hospitalini Jijini London asubuhi ya leo.

Taarifa hazijasema zaidi juu ya sababu za kifo chake,hata hivyo mwaka 2015 alipata stroke iliyomfanya awe hospitalini kwa muda mrefu sana.

Agogo takumbukwa na wengi hasa katika michuano ya Mataifa Afrika (African cup of Nation) mwaka 2008 na amefariki akiwa na umri wa miaka 40.

#RIP regend


Wednesday, August 21, 2019

YAWEZEKANA TANZANIA KUPATA ARENA YA KIKAPU

Inawezekana kabisa kupata Uwanja wa aina hii .

 Uwanja wa kisasa kwa matukio makubwa  ya kikapu , ngumi na maonesho mbalimbali   . ikiwa Nchi ya Rwanda wamefanikiwa kwenye hili.


Nazani hata Tanzania kama itakuwa tayari kwa hili inaweza fanikiwa kupata Arena kama hii kubwa ya kisasa kwa ajiri ya maendeleo ya mpira wa kikapu nchini