Entertainment

Local News

International News

Video

Drake akanusha uvumi kuwa amemchumbia Serena Williams

Kuliibuka uvumi kuwa rapper Drake amemchumbia mcheza tennis mahiri Serena Williams ambaye inaaminika kuwa wanauhusiano licha ya kuwa wao binafsi hawajathibitisha.
drake-serena
Baada ya taarifa hiyo kusambaa mtandaoni jana, mwakilishi wa Drake aliiambia TMZ kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.
Jarida la OK liliandika story Alhamisi hii kuwa Drake alimchumbia Serena walipoenda Canada nyumbani kwao Drake, na kuwa Serena alisema ‘Yes’ laikini walipanga kuweka mambo kimya kimya kwa sasa.
0824-drake-serena-williams-launch3-3
Drake (28) na Serena (34) wameonekana kuwa karibu sana kwa miezi sasa, kitu kinachoashiria kuwa wamezama kwenye dimbwi la mapenzi.

Msanii wa Nigeria Runtown awataja wasanii wawili wa Tanzania anaowakubali zaidi


Mwimbaji kutoka Nigeria, Runtown ametua jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo (Oct.9) tayari kulipamba jukwaa la fainali ya shindano la kusaka vipaji Bongo Star Search (BSS) itakayofanyika Ijumaa (Oct.9).
runtown (1)
Kama ambavyo wasanii wetu wanafuatilia kwa karibu muziki wa Nigeria, Runtown pia anafatilia muziki wa Bongo. Katika mahojiano mafupi na Fahamu Tv, Runtown amewataja wasanii wawili wa Bongo anaowakubali zaidi. Alianza kumtaja hit maker wa ‘No Body But Me’ Vanessa Mdee kwa upande wa wasanii wa kike, pia akamtaja Diamond na kusema kuwa ndiye msanii namba moja anayemkubali zaidi kwa wasanii wa kiume wa Tanzania.
Runtown pia amethibitisha kuwa amefanya collabo na Chege, na kuongeza kuwa kuna collabo nyingine atakazofanya na Diamond na Vanessa.

NAMNA AMBAVYO WAFANYAKAZI MNAWEZA KUGOMA KISHERIA.


   bashiryakub.blogspot.com
Na  Bashir  Yakub.
MARA  kadhaa  migomo  ya wafanyakazi imekuwa  ikizaa athari  mbaya kwao. Hii  ni  kutokana  na  kugoma  bila  kufuata  taratibu. Waajiri  wao  ni  wajanja. Huwa  makini  sana linapoibuka  wazo  la  kugoma  na  huwa  tayari  muda  woote  kufuatilia  nyendo  ili  panapo  kosa  kidogo  watumie  mwanya  huo  kuwadhibiti   wagomaji.  

Na  kikubwa  wanachofanya hali  ikishakuwa  hivi  ni   kusema  mgomo  haukuwa  halali  na  hapo  kupata  nafasi  ya  kuwashugulikia  waliohusika  katika  kugoma mmoja baada  ya  mwingine.  Katika  mazingira  kama  haya  ni  vema  wafanyakazi  kufahamu  taratibu  za  kisheria  zinazohusu  mgomo  ili  wakati  wa  kufanya  hivyo  asitokee yeyote  kati  yao  wa  kuathiriwa  na  ugomaji  huo.

1.SHERIA  INAMRUHUSU  MFANYAKAZI  KUGOMA.
Wapo  wanaodhani  kugoma  ni  uasi.  Kwa  mfanyakazi  hili  si  kweli.  Kugoma  ni  haki  ya mfanyakazi  kama  zilivyo  haki nyingine.  Kama  ilivyo    haki  ya  kupokea mshahara,  haki  ya kulipwa  muda wa  ziada,  haki  ya muda  maalum  wa  kufanya  kazi, likizo  na  haki  nyinginezo   kwa  ujumla  wake. Kugoma  si  dhambi   isipokuwa  takwa  halali  la  kisheria.  Kitaalam  mgomo  wa  wafanyakazi  huitwa  “strikes” .  Ni  hatua  ambapo  wafanyakazi  hugomea  kuingia  maeneo  ya  kazi  au  huingia  maeneo  ya  kazi  lakini  wasitoe  huduma  kama  ilivyo  ada yao.  

Kisheria  kugoma  ni  jukwaa  la  kuitisha  mjadala  wa  kujadii  maslahi  ya  kazi  kati  ya  mwajiri  na  mwajiriwa.  Kugoma  ni  Jambo  halali  kisheria  ndicho  ninachotaka  kusema  na  kuwatoa  hofu  baadhi  wajuao  kugoma  ni  uasi  na  usaliti.Na haya  ni  kwa mujibu  wa kanuni  namba  ya 42,sheria  namba 6 ya  ajira  na  mahusiano  kazini.

2.  WAFUATAO  HAWARUHUSIWI  KUGOMA.
Makundi  ya  wafanyakazi  watoao  huduma  muhimu  katika  jamii  migomo  kwao  imeharamishwa.  Huduma  muhimu  katika  jamii   hutegemea  na  mahitaji  ya  jamii  husika. Yumkini  hapa  kwetu  huduma muhimu  katika  jamii  hujumuisha watumishi  katika  idara  za  afya, maji  safi  na  salama,  nishati  na  umeme,  vyombo  vya  ulinzi  na  usalama, zimamoto  na  watoa huduma  ya  kuongoza  ndege.  Sababu  kubwa  za  kuzuia  makundi  haya  kugoma  ni  kuwa  kugoma  kwao  huweza kuleteleza  hasara  ambazo  kwazo  haziwezi  kufidiwa  na  kitu  chochote    baada  ya  kutokea kwake.  Na   hasara  kubwa zaidi  hapa  ni  vifo  na  ulemavu  wa  kudumu vitu  ambavyo  haviwezi  kufidiwa  kwa  namna  yoyote na  kitu  chochote .

3.  WANAOTAKA  MGOMO  HALALI  WAFUATE  UTARATIBU  HUU.
( a ) Kwanza  kabisa  hakikisheni  mgomo  wenu  unahusu  maslahi  ya  kazi  yenu.  Usiwe  mgomo  ambao nyuma  yake  wako  watu  hasa  wanasiasa  wanaowasukma  ili  kutimiza  haja  zao fulani. Au  usiwe  mgomo  ambao  umeandaliwa  lengo  likiwa  kumkomoa  mwajiri.  Ni  lazima  kuwepo  na  nukta   muhimu  na  ya  wazi  kabisa  inayohusu  maslahi  katika  kazi  yenu.
( b ) Kabla  ya  kugoma  lazima  muwe  mmepitia  hatua  ya  usuluhishi( mediation). Na  mnapokuwa  mmepitia  hatua hii  ni  lazima  iwe  imethibitika  kuwa  hatua  hiyo  imeshindwa  kutatua  mgogoro  wenu  na  sasa  hatua  inayofuata  ni  ya  kugoma.  Ikiwa  hatua  ya  usuluhishi  imefanikiwa  na kutoa  majawabu    ya  mgogoro  itakuwa ni  haramu  kwa yeyote  kugoma. Kugoma  ni  pale  tu  hatua  ya  usuluhishi  inaposhindwa   na  hatua  hii  hutakiwa  kuchukua  muda  wa  siku  thelathini. Ni  muda  huo utakaotumika  kutafuta  muafaka  kabla  ya  kutangaza  mgomo.
( c ) Ikiwa  mgomo  utakuwa  umeitishwa  na  chama  cha  wafanyakazi  basi kura  za  wengi  ndizo  zitakazotoa  ruhusa  ya  kugoma. Ikiwa  wengi  watakataa  basi  hakuna  mgomo.
( d ) Baada  ya usuluhishi  kushindikana  wafanyakazi  wanaolenga  kugoma  watatakiwa  kutoa  taarifa(notice)   ya  masaa  48  sawa  na  siku  mbili kwa  mwajiri   kabla ya  kuanza  kugoma. Ni baada  ya  muda  huo  ndipo mgomo  utaanza.
( e ) Ikiwa mgomo  utaahirishwa  baada  ya  masaa  48  yaliyokuwa  yametangazwa  kupita,  basi   kama  mnatarajia   kuendelea  na  msimamo  wa  kugoma  mtatakiwa  kutoa  muda mwingine  wa  masaa  48.
Kama  wafanyakazi watafuata  utaratibu  huu  kugoma   hakuna  madhara  yoyote mabaya  yatakayotokea  kwao ikiwa  ni  pamoja  na  kutishiwa  kufukuzwa  kazi.
MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

RAIS NYUSI WA MSUMBIJI AMWANDALIA JK DHIFA MAALUM YA KUMUAGA, JIJI LA MAPUTO LAMTUNUKU UKAZI WA KUDUMU


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi  wa Msumbiji wakigonga glasi ya kutakiana heri wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo jijini Maputo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa Msumbiji akisisitiza kuwa uhusiano wa kidugu na kipekee kati ya nchi hizo mbili utaendelea kudumu na kukua
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wakisimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akimvisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete vazi maalum na kumkabidhi Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo

 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akijiandaa kumpa  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo.

MKUU WA MKOA WA MWANZA KUSHIRIKI ROCK CITY MARATHON

 Katibu wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani (wa pili kushoto), akipokea fomu ya usajili kutoka kwa Katibu wa chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (wa pili kulia), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na Mratibu wa mbio za Rock City Marathon kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi. Adella Lamsa (kulia).
 Katibu wa idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani, akisaini fomu ya usajili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye jana alijisajili rasmi kushiriki katika mbio za kilomita tano katika mbio za Rock City Marathon zinazotarajia kufanyika tarehe 15 Novemba, 2015 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wanaoshuhudia ni Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Mwanza, Kizito Bahati (kushoto) na Katibu wa chama cha riadha Mwanza, Peter Mujaya (kulia).
Na mwandishi wetu
Ikiwa ni siku chache kupita baada ya uzinduzi wa mbio za Rock City Marathon 2015, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo amekua mtu wa kwanza kujisajili kushiriki mbio hizo zilizopangwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizindua usajili wa ushiriki wa mbio hizo jijini Mwanza jana, Mulongo, aliyewakilishwa na Katibu idara ya utumishi wa waalimu mkoa wa Mwanza, Bw. Genzi Sahani, alitoa  wito kwa wanariadha nchini kujitokeza kwa wingi ili kuongeza ushindani wa mbio za mwaka huu, ambazo zimekuwa na lengo la kuhimiza utalii wa ndani nchini.

 “Nimekuwa mfuatiliaji wa mbio hizo tangu zilipoanzishwa mwaka 2009 na tumeshuhudia viwango vya mbio hizi vikipanda kila mwaka, kitu ambacho ni kielelezo cha kuonyesha maandalizi mazuri yanayofanywa kwa kuzingatia viwango na sheria zilizo wekwa,” alisema Mulongo katika shughuli hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha.

Mulongo, alisema kuwa katika miaka ya hivi karibuni mchezo wa riadha umekua ukififia na kutaka wadau mbalimbali, ikiwemo makampuni binafsi, kuunganisha nguvu ili kuurudisha kwenye ramani mchezo huo ulioliletea taifa sifa kubwa katika miaka ya nyuma.

“Ni kweli kwamba makampuni na hata watu binafsi wanajitokeza kusaidia kukuza mchezo wa riadha hapa nchini, lakini bado mchezo huu una changamoto nyingi hususani katika mkoa wetu wa Mwanza na bado zinahitajika jitihada za ziada kwa wadau mbali mbali wa mchezo huu kushirikiana ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi bila kusahau viongozi wa chama cha Riadha Mkoani Mwanza,” alisema.

Akizungumza katika shughuli hiyo, Meneja wa Shirika la hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Mwanza Shaaban Luanda, ambao ni wadhamini wakuu, alisema: “Mbio za Rock City Marathon zimekuwa na mchango mkubwa katika kuinua mchezo wa riadha nchini. Sisi kama shirika la hifadhi ya jamii tunaamini kupitia michezo tunaweza kulinda afya ya jamii na ndio maana tumeendelea kudhamini mbio hizi.

Follow me instagram pascal_mzee_wa_chimbo